Mpendwa Mwanachama,
Ni matumaini yetu una afya njema na unaendelea na shughuliza zako za kila siku,
Kumekuwa na utaratibu wa mawakili kupata adhabu ya asilimia Hamsini ya ada ya Mahakama pale ambapo wanachelewa kuhuisha leseni zao. Adhabu hii imekua ikitolewa kuanzia tarehe 01 mwezi Februari kila mwaka.
Kutokana na kuwekwa kwa adhabu hii kinyume na Kanuni ya 5 ya Advocates (Admission and Practising Certificate ) Regulations GN No. 62 ya mwaka 2015, Mtendani Mkuu wa TLS amefanya kikao na Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama tarehe 31 Januari,2024 katika ofisi ya Msajili Mkuu wa Mahakama, Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili swala hili ili kuona namna gani adhabu hii inaweza kutozwa kwa mujibu wa kanuni hii na si vinginevyo.
Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu kuwa, Mhe. Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama amelipokea swala hili na kuahidi kulifanyia kazi kwa kulifikisha kwa uongozi wa juu wa Mahakama kwa marekebisho au muongozo zaidi. Mhe Kaimu Msajili Mkuu wa Mahakama, ameahidi kutupa mrejesho wa swala hili mapema iwezekanavyo ili Mawakili wasiendelee kutozwa adhabu hii kinyume na kanuni na kuhakikisha taratibu za kuhuisha leseni ya uwakili zinafata mwongozo uliowekwa katika Kanuni ya 5 ya Advocates (Admission and Practising Certificate ) Regulations GN No. 62 ya mwaka 2015.
Nawatakia mafanikio mema katika majukumu yenu.
Regards,
|Tanganyika Law Society Secretariat
|Plot No. 391|Chato Street|Regent Estate |P.O. Box 2148, Dar es Salaam, Tanzania; Tel: +255 222775313
Leave A Comment