UWEPO WA VISHOKA WASIO MAWAKILI NA MAWAKILI WASIOHUISHA LESENI ZAO

Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kinapenda kukutaarifu uwepo wa watu wanaofanya kazi za uwakili bila kuwa wanataaluma wa tasnia hiyo (vishoka), pamoja na uwepo wa mawakili ambao ni wataalamu wa tasnia hiyo lakini hawajahuisha leseni zao hivyo kukosa sifa za kuwajibika kikazi kama mawakili halali mpaka hapo watakapohuisha leseni zao.

Hivyo tunakutahadharisha kuwa makini pindi unapohitaji Wakili wa kukuwakilisha katika masuala mbalimbali ya kisheria haswa uwakilishwaji Mahakamani, katika Mabaraza, kushuhudia viapo, ugongaji wa mihuri ya wakili katika nyaraka na huduma nyingine zinazohitaji wakili.

Madhara ya kuwatumia mawakili ambao hawajahuisha leseni zao za uwakili na watu wasio na sifa ya kufanya kazi ya uwakili ni; kazi yoyote aliyoifanya wakili huyo au mtu huyo haitatambulika kisheria, kupoteza fedha ulizomlipa wakili huyo au mtu huyo, kupoteza muda wa shauri lako na kupelekea kufutwa Mahakamani, pamoja na kuharibu shauri lako au kesi ambayo ilikuwa ina mwenendo mzuri.

Aidha; tunapenda kuutaarifu Umma kuwa, kabla hujampatia kazi yoyote wakili au mtu yeyote anayesema yeye ni wakili, hakikisha kama mtu huyo ni wakili kweli na ana leseni halali ya uwakili (amehuisha leseni yake) kwa kufuata utaratibu ufuatao;-https://tams.judiciary.go.tz/sw/

  1. Ingia katika tovuti ya Mahakama iitwayo “TAMS” au ‘Mfumo wa Mawakili Tanzania’ kwa ‘link’ hii
  2. Ukishafungua utakutana na kipengele kiitwacho “MJUE WAKILI” utaandika jina la wakili kupata uthibitisho wa wakili huyo.
  • Endapo jina la Wakili huyo HALITATOKEA, basi mtu huyo si Wakili ni kishoka hivyo basi usimuhusishe katika masuala yako ya kisheria kwani ni kosa la jinai, unatakiwa kumripoti katika kituo cha polisi chochote kilicho karibu na wewe.
  1. Endapo katika kuthibitisha utakuta jina la Wakili limetokea lakini ameandikiwa “HARUHUSIWI’’ tambua kuwa Wakili huyo hajahuisha leseni yake ya uwakili hivyo haruhusiwi kufanya kazi zozote za kiuwakili hadi atakapohuisha leseni yake. Usimuhusishe Wakili wa aina hiyo katika masuala yako yoyote ya kisheria kwani kwa kufanya hivyo chochote kile atakachokifanya hakitatambulika na kitakuwa batili kisheria.
  2. Endapo utakutana na jina la Wakili lakini chini yake limetokea neno “HAFANYI KAZI YA UWAKILI” huyo ni Wakili lakini kwa sababu maalum zinazotambulika kisheria haruhusiwi kufanya kazi yeyote ya uwakili, unashauriwa usimuhusishe katika masuala yako ya kisheria.
  3. Endapo utakutana na jina la Wakili na chini ya jina la huyo Wakili imeandikwa “ANARUHUSIWA” basi huyo ni Wakili aliyehuisha leseni yake ya uwakili na anaruhusiwa kufanya kazi ya uwakili hivyo unaweza kumuhusisha Wakili huyo katika masuala yako ya kisheria.

Tunatoa Onyo kali kwa wale wote wanaojihusisha na masuala ya uwakili wakati si mawakili (vishoka), kwani kwa kufanya hivyo unawasababishia wananchi wengi kukosa haki zao za kisheria. Hivyo tunawataarifu waache vitendo hivyo mara moja na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na hujuma hii.

Pia tunatoa wito kwa yeyote atakayekutana na Kishoka asisite kutoa taarifa kituo chochote cha polisi, au piga simu namba hii:

0779-6262699.

Imetolewa na:

 CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)

 

Calendar
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  

Get In Touch

Latest Posts

Shopping Cart

No products in the cart.