TLS YAWEZESHA KIKAO CHA KAMATI YA MKOA YA URATIBU WA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA KATIKA MKOA WA MOROGORO.

Mapema leo, TLS imewakutanisha wajumbe wa kamati hii na kujadili kwa pamoja mipango mikakati ya kuimarisha na  kuleta ufanisi katika huduma ya msaada wa kisheria kuanzia ngazi ya jamii na kuhakikisha huduma hiyo inamfikia muhitaji kwa wepesi na kwa ubora stahiki.

Kamati hiyo imejadili kwa mapana kazi za kamati ambazo ni pamoja na;-

  • Kuimarisha ushirikiano na mahusiano miongoni mwa wadau wanaojishughulisha na masuala ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria,
  • Kuimarisha uwezo wa wadau katika ngazi zote, kuwezesha na kusaidia huduma ya msaada wa kisheria inayotolewa na wadau.
  • Kutumia vyombo vya habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusu upatikanajki wa msaada wa kisheria na kuhamasisha jamii juu ya masuala ya haki.
  • Kubuni mbinu na mikakati itakayowezesha upatikanaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi katika ngazi ya chini kwa urahisi na wepesi.
  • Kushiriki, kuandaa na kutekeleza maadhimisho ya kitaifa, kikanda, kimkoa yenye lengo la kuwafikia wahitaji kwa wingi na kwa muda mfupi.
  • Kufanya ufatiliaji na tathimini ya shughuli za msaada wa kisheria katika ngazi za mkoa na halmashauri ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma za kisheria unatolewa kwa mujibu wa Sheria za Msaada wa kisheria Na. 1 ya 2017, pamoja na kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa chini ya sheria.

Wajumbe wa kamati hiyo waliohudhulia ni pamoja na  Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (NPS), Afisa kutoka Dawati la Jinsia la Polisi, Afisa kutoka Jeshi la Magereza, Wawakilishi wa wadau wa Mawendeleo, Afisa Ustawi wa Jamii ngazi ya Wilaya, Muwakilishi wa Chama cha Mawakili Tanganyika ngazi ya mkoa Bwana Godfrey G Mwansoho ambae kikao hiki kimemteua kuwa mwanyekiti wa kamati hiyo, wadau wengine ni pamoja na Viongozi wa Dini, Muwakilishi wa Vyombo vya Habari, vyombo vya habari pamoja na Msaidizi wa Msaada wa kisheria.

Wadau hawa wametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanajenga mazoea ya kuyapeka matatizo yao madogomadogo katika ngazi za awali ambazo ni za wasaidizi wa kisheria ili wapate huduma hiyo bure kwani wengi wamekuwa wakikimbilia kufungua kesi Mahakam hata katika masuala madogo ambayo yangeweza kuamuliwa na kusuluhishwa na wasaidizi wa kisheria

Ili kuwapata wasaidizi wa kisheria, fika katika ofisi ya Kijiji, kata au wilaya, ulizia wasaidizi wa kisheia na utapata msaada!

WAKILI TV- KITOVU CHA SHERIA!

 

Calendar
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  

Get In Touch

Latest Posts

Shopping Cart

No products in the cart.