TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA VIRUSI VYA CORONA (COVID _19) NA MABADILIKO KATIKA UTOWAJI WA HUDUMA  

Ndugu mwanachama wa Chama cha Mawakili Tanganyika,  Mwananchi na Mdau wetu;
Kutokana na idadi  ya maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kuzidi kuongezeka, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kinatoa wito kwako kuzidi kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu ambapo mpaka sasa,   unazidi kuenea ulimwenguni  kote kwa kasi kubwa, vifo vinazidi kuongezeka  na kinga au  tiba yake bado haijapatikana.
TLS imeamua kuchukua tahadhari na hatua zaidi katika kupambana na ugonjwa huu kwa kuulinda umma,  wanachama wake, wafanyakazi na wadau wengine kwa ujumla:

Tahadhari na Kujikinga dhidi ya Corona (COVID-19)
Ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya hatari katika kupambana na kujikinga na ugonjwa huu  kwa kufanya  na kuzingatia yafuatayo:
(i)                 Kuepuka sehemu za Mikusanyiko.
(ii)               Kuepuka safari au mizunguko isiyo ya lazima,
(iii)             Kunawa Mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara,
(iv)             Kutumia Vitakasa Mikono (sanitaizer),
(v)               Kula mlo kamili na kula vyakula vyenye vitamin C kwa wingi ili kuimarisha kinga ya mwili,
(vi)             Kufanya Mazoezi ili kuhimarisha afya kamili,
(vii)           Kuzingatia  kikamilifu maelezo ya maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya au Serikali, na
(viii)         Kwenda kituo cha afya au kutoa taarifa pale utakapokuwa  au utakapomuona mtu mwenye  dalili za ugojwa huu kama vile mafua makali, homa kali, kushindwa kupumua vizuri, maumivu ya kichwa na dalili zingine zilizo elezwa na Wizara ya Afya.

Pamoja na kuushauri umma, wanachama na wadau wetu  kuchukua tahadhari na kujikinga na ugonjwa huu, Chama pia kimechukua hatua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huu katika mazingira yake ya kazi  kama ifuatavyo:

Kusitisha shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko

TLS imesitisha shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko ya watu ikiwemo semina (CLEs), mikutano na warsha  mpaka hapo ambapo mamlaka husika zitakapotangaza kuwa ni salama kuendelea na shughuli hizi.
Vikao vya Kamati pamoja  na Baraza la Uongozi la Chama

Vikao vya kamati zote za chama pamoja na vikao vya Baraza la Uongozi la Chama vitafanyika  kwa njia ya kieletronikia.
Huduma za Msaada wa Kisheria na Maswala ya Kimaadili dhidi ya Mawakili

Huduma hizi zitaendelea kutolewa kama kawaida kwa kufuata utaratibu ufuatao:
(i)                 Huduma hizi zitatolewa kwa siku za Jumanne na Alhamisi tu kwanzia saa Nne asubuhi hadi saa Nane mchana.
(ii)               Mteja anatakiwa kuleta nukushi ya nyaraka zake ( photocopy) zikiwa katika bahasha.
(iii)             Mteja atapewa fomu ya maelezo ambayo atajaza taarifa zake na maelezo ya shauri lake kwa ufupi. Fomu hiyo itapatikana mapokezi
(iv)             Baada ya kujaza fomu hiyo mteja ataingiza ndani ya  bahasha aliyokuja nayo yenye nukushi za nyaraka zake na kuweka katika sehemu maalum atakayoelekezwa.
(v)               Mteja atapewa namba ya simu  au barua pepe kwa ajili ya mawasiliano zaidi kuhusu shauri lake.
(vi)             Mteja hataruhusiwa kuonana ana kwa ana na afisa wa msaada wa kisherai au afisa maadili   mpaka pale atakapopigiwa simu.
Utolewaji wa Vitambulisho kwa Wanachama

(i)                 Vitambulisho vya mawakili  waliopo mikoani vinaendelea kutolewa na viongozi wa chapter kama ilivyokuwa mwanzo.  Mawakili wa mikoani mnaombwa kuwasiliana na viongozi wenu wa chapter watawaeleza utaratibu , muda na mahali pa kuchukua vitambulisho vyenu.
(ii)               Kwa mawakili waliopo Dar es Salaam vitambulisho vitatolewa kwa siku ya Jumanne na Alhamis tu  kwanzia saa Nne asubuhi hadi saa Nane Mchana. Mwanachama anatakiwa kufika kuchukua kitambulisho chake pale tu atakapopokea ujumbe wa SMS kuwa kitambulisho chake kipo tayari. Mwanachama akishapokea SMS kuwa kitambulisho chake kipo tayari, anatakiwa kuja kukichukua katika siku na muda uliopangwa  hapo juu.

Tunawasisitiza wanachama kujaza taarifa zao za Chapter walizopo kwenye akaunti zao za Wakili Data Base. Kitambulisho hakiwezi kutengenezwa kama taarifa za mwanachama hazijajazwa au hazijakamilika.

Sekretariat

Kutakuwa na wafanyakazi wachache watakaofika ofisini kwa  utaratibu wa zamu  kutoa huduma kutokana na maagizo yaliyotolewa na Mamlaka (Serikali na Mahakama). Wafanyakazi hao watafika katika muda uliopangwa kila siku. Hata hivyo,  wafanyakazi waliopo zamu watachukua tahadhari zote za kujilinda na ugonjwa huu ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vitakasa mikono (sanitaizer), kuvaa barakoa, na kupimwa joto la mwili kabla hawajaingia ofisini na kutekeleza majukumu yao. Wafanyakazi wengine wataendelea kufanya kazi wakiwa nyumbani au mahali pengine popote kulingana na majukumu.
Huduma Zingine kwa Umma ,Wanachama na Wadau Wengine Katika ofisi ya Makao Makuu

Huduma zingine kwa umma, wanachama  na wadau wengine zitaendelea kutolewa  kwa njia za mtandao kwanzia saa Nne asubuhi hadi saa Nane Mchana . Hata hivyo tunaomba wanachama wetu , wananchi na wadau wengine kwa ujumla, kwa huduma ambazo sio za lazima kufika katika ofisi zetu kutumia nyia nyingine za mawasiliano kama  simu au barua  pepe.
( Zingatia: Muda wa kupiga simu ni kwanzia saa Nne Asubuhi hadi saa Nane  Mchana siku za Kazi)

Zifuatazo ni njia za mawasiliano na wahusika kamili:

(i)                 Mapokezi  na Huduma za Utawala Piga simu Na. 0777815757 au  0778120424  email info@tls.or.tz
(ii)               Vitambulisho piga simu No. 0779939038 plubuva@tls.or.tz
(iii)             Msaada ya Kisherai simu Na. 0778626212 mwingwaj@gmail.com
(iv)             Semina na CLE 0779626281 rsalvatory@tls.or.tz
(v)               Malipo ya Ada, Risiti na matatizo yote yanayohusu malipo  piga Simu Na. 0778626212 vmbuligwe@tls.or.tz
(vi)             Malalamiko ya Kimaadili dhidi ya Mawakili  0779626299 vswai@tls.or.tz
(vii)           Huduma zingine za wanachama 0778626286 amuro@tls.or.tz
(viii)         Huduma za Machapisho  Na. 0779626280 publication@tls.or.tz
Huduma Zingine kwa  Wanachi , Wanachama na Wadau wengine Katika Ofisi Zetu za Mikoani (Chapters)

Huduma zingine kwa umma, wanachama  na wadau wengine zitaendelea kutolewa mikoani siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kwanzia saa Nne asubuhi hadi saa Nane Mchana.  Kwa wateja wa msaada wa kisheria na malalamiko ya kimaadili dhidi ya mawakili utaratibu utakuwa ule ule wa kupokea nyaraka  (nukushi) kama ilivoainishwa hapo juu.
Kwa huduma ambazo sio lazima kufika katika ofisi hizo  zitatolewa kwa njia ya mawasiliano ya simu na barua pepe
( Zingatia: Muda wa kupiga simu ni kwanzia saa Nne Asubuhi hadi saa Nane  Mchana siku za Kazi)

Zifuatazo ni njia za mawasiliano na wahusika kamili:
Mwanza   0713501134 tlsmwanzachapter@gmail.com
Mbeya     0779626216 au 0755626442 mbeyachapter@tls.or.tz
Arusha     0779626219 , 0712762799 arushachapter@tls.or.tz
Dodoma   0779626215 au 0779626221 dodomachapter@tls.or.tz , mkessy@tls.or.tz
Mtwara     0765030889   fawasi@tls.or.tz , mtwara@tls.or.tz

Kwa Mawakili, wanachi na wadau wengine  walipo mikoa  ambayo haijatajwa hapo juu wanaweza kupiga simu moja kwa moja kwenye namba za kipengele namba 5 (cha makao makuu) au kuwasiliana na viongozi wao wa chapters.
Chama kitaendelea kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli zake kwa kuzingatia hali na mwenendo wa maambukizi ya virusi hivi vya Corona pamoja na taarifa zitakozokuwa zikitolewa na mamlaka husika.

Chukua Taadhari, Kabla ya Hatari

Tangazo hili limetolewa na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS)

Regards,

|Tanganyika Law Society Secretariat

Calendar
August 2022
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  

Get In Touch

Latest Posts

Shopping Cart

No products in the cart.