Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Hakimu Mkazi Daraja la II – (TJS 2) nafasi 100, Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 20, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – (TGS B) nafasi 45, Mpokezi – (TGS A) nafasi 1, Dereva Daraja la II – (TGOS A) nafasi 10, Mlinzi (TGOS A) nafasi 21 na Afisa TEHAMA Daraja la II Nafasi 3 (TGS.E). Bonyeza hapa NAFASI ZA AJIRA-TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA (LATEST)

You may also like

Leave A Comment

Please enter your name. Please enter an valid email address. Please enter message.