Katika kutekeleza mradi wa SIRD (Supporting Inclusive Resource Development in East Africa) Tanganyika Law Society imeendelea na mkutano wa siku tatu wa kitaifa unaomalizika leo. Mada kuu za leo zikiwa ni mgawanyo wa Mapato katika sekta ya madini, pamoja na mchango wa TLS katika kuhakikisha masula ya kisheria yanatekelezwa ipasavyo.

Haya ni baadhi ya maoni ya wadau katika mada ya mgawanyo katika sekta ya madini;

Mgawanyo sahihi wamapato kutokana na uzalishaji wa bidhaa za viwanda na madini huchangia ukuaji wa uchumi kwa nchi na maendeleo ya kasi. Sera na sheria za mgawanyo wa mapato kutokana na uzalishaji wa bidhaa za viwanda na madini ni muhimu kupitiwa mara kwa mara na kufanyiwa marekebisho, uchumi hubadilika mara kwa mara duniani ~ Richard Lane

Katika kuweka uwazi wa kinacho patikana kwenye uchimbaji wa madini tumekuwa tukifuata sheria za nchi na kupitia sera mara kwa mara ili kuboresha pale inapoonekana kuna malamiko. Kwa kiasi kikubwa Geita Gold Mining (GGM) imekuwa ikijihusisha katika kuangalia jamii inayo zunguka mgodi inanufaika na rasilimali madini na tumekuwa tukifanya vikao vingi na wananchi kujenga maridhiano, 2012 Geita Gold Mine (GGM) tulianzisha Mradi wa Maji kutoka ziwa Victoria kwa makubaliano ya Kujenga, kusafisha maji na kuhakikisha yanawafikia wananchi wa Geita huu ni mradi ambao haujakamilika ila angalau kuna wanachi wanapata Maji~ Mr Manace Ndoroma

Changamoto kubwa kwa jamii yetu ni elimu ndogo na hii huchangia wananchi wa jirani na mgodi kutokupata kazi za kitaaluma tunashukuru mgodi kwa kuendelea kujenga shule ~ Fortunata Mutisha. Pia tumegundua wananchi hafuatilii habari zinazowekwa kwenye mitandao juu ya uzalishaji na ugawanyaji wa mapato ya madini, mafuta na gesi na huwa wanafahamu kijuu juu ~ Raphael Mgaya

Tumejitahid kuandaa majarida na kufanya midahalo,mikutano mbalimbali na wananch wanao zunguka migodi kuwaelimisha juu ya kuepuka madhara ya kemikali mgawanyo wa mapato na sheria za kazi ~ Godfreya Keraka

Haya ni majidiliano yanayoendelea katika mkutano wa kitaifa unaofanywa na mradi wa SIRD unaotekelezwa na Tanganyika Law Society. Msaada wa kisheria katika utekelezaji wa majukumu ya sekta za madini umeonesha chachu ya jinsi gani sharia ikifuatwa itaboresha si tu maisha ya waliozunguka migodi bali pia mahusiano kati ya jamii na wawekezaji pamoja na serikali katika eneo husika.

Tanganyika Law Society inahitimisha mkutano huo iliochukua siku tatu katika ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam kwa kubainisha wajibu wake katika sekta ya madini, mafuta na gasi ikiwa ni pamoja na Kusimamia haki za binadamu,  Kutengeneza sheria juu ya usimamizi uwazi uwajibikaji na mgawanyo wa rasilimali kwa kushirikiana na serikali. leo ni kuwafanya wadau wetu ambao ni wananchi, wawekezaji na serilkali unufaika na miradi hiyo.

You may also like

Leave A Comment

Please enter your name. Please enter an valid email address. Please enter message.