UFAFANUZI WA MWONGOZO WA MAWAKILI KUWAONA MAHABUSI MAGEREZANI
Wizara inapenda kukujulisha kuwa utaratibu uliopo kwa mujibu wa sheria na taratibu unatoa fursa kwa watu wote wakiwemo mawakili kuwaona wateja wao (Wafungwa/Mahabusu)katika siku za Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu. Aidha, ili kuweza kuwaona wafungwa/mahabusu katika siku za kazi (Jumatatu -Ijumaa) utahitaji kibali maalum ambacho huombwa kwa Mkuu wa Gereza.
Kwa maelezo hayo, tunapenda kukujulisha kuwa Wizara kupitia jeshi la Magereza itaendelea kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanzania katika kuwezesha kuwaona wateja wao kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria pale inapohitajika.
Tunashukuru kwa ushirikiano wako.
Regards,
|Tanganyika Law Society Secretariat
Leave A Comment