Mkutano mkuu wa chama cha wanasheria Tanganyika Bara ulifanyika tarehe 13 & 14/04/2018 katika ukumbi wa mkutano wa Mt Meru Hotel jijini Arusha na kuhudhuriwa na Mawakili takribani elfu moja na mia tisa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara. Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali. Pamoja na mengi aliyoyazungumzia mgeni rasmi, alisisitiza uwajibakaji na uadilifu. Jaji Wambali alizindua kitabu kipya (Law Report 2017) ambacho hutolewa kila mwaka na Chama cha wanasheria Tanzania Bara (TLS).

Uchaguzi wa viongozi mbalimbali 2018/2019 ikiwa ni pamoja na uraisi, makamu wa raisi, mhasibu pamoja na baraza la uongozi wa chama hicho ulifanyika. Fatma Karume aliibuka mshindi wa nafasi ya Uraisi, Rugemeleza Albert Nshala makamu wa raisi, na Nicholaus Muntumba Duhia akiibuka mhasibu wa chama chicho. Kamati ya Uongozi wa TLS itawakilishwa na Aisha Ally Sinda, Godluck Walter, Geremia Mtobesya, Jebra Kambole, Lambaji Madai, Magdalena Sylister na Stephen Axwesso.

Zoezi jingine muhimu katika mkutano huo ilikuwa ni vikao(forums) mbalimbali ikiwemo foram ya wanawake (Women Lawyers’ Forum), foram ya vijana (Young & Junior Lawyers’ Forum) pamoja na foram ya wanasheria wa kujitegemea (Law Firm Forum). Mafunzo pamoja na mijadala mbalimbali yalitolewa na wabobezi wa masuala ya kisheria lengo likiwa ni kuhakikisha kila idara inazikabili changamoto zake na kuzifanyia kazi.

Mkutano mkuu ulidhaminiwa na wadau mbalimbali wa chama hicho ikiwemo Ngorongoro Conservation, Thomson Reuters, TAWLA, ABC Attornery, AHQ SPECHT, ASLAY Attornery, APEX, EALS, PRECISION Air, Air Tanzania, TOTAL, GPITG, Freedom House, Simba Ngilimi & Associates Advocates, IMMMA Advocates, LSF, Okoa Muda na WDHOCK Lager. Kwa dhati, Tanganyika law Society inawashukuru sana na kuhimiza ushirikiano wa kibiashara kwa manufaa ya wote.

You may also like

Leave A Comment

Please enter your name. Please enter an valid email address. Please enter message.