User avatar
tlsadmin
Posts: 8
Joined: Feb 2, 2015 07:02:18

Ubora na Mapungufu ya Katiba Iliyopendekezwa

Nov 24, 2015 00:11:00

Mawakili wasomi,

Tukiwa manguli wa sheria hapa nchini, tunawajibu wa kutumia taaluma yetu kuwaelimisha wananchi na kushawishi maboresho (kama yapo) kwa katiba iliyopendekezwa kwa mustakabali wa taifa letu.

Tungependa kupata maoni yako binafsi kwa kuzingatia taaluma yako na bila kufungwa na itikadi za chama cha siasa au dini juu ya nini ubora na mapungufu ya katiba iliyopendekezwa.

User avatar
Novat
Posts: 1
Joined: Mar 11, 2015 15:03:22

Re: Ubora na Mapungufu ya Katiba Iliyopendekezwa

Nov 25, 2015 00:11:00

Hii ni hoja mujarabu, na inaakisi kipindi tulichomo sasa.
Maoni yangu ni kuwa katika utangulizi wa kuelimisha yaliyomo, inafaa kueleza japo kwa ufupi kuwa palikuwepo makosa ya kisheria katika hatua za Mchakato Katiba Mpya. Ibara ya 98 ilipaswa ifanyiwe kwanza merekebisho ili kutoa uhalali wa kuhuisha katiba.

Pungufu kubwa sana kwa Katiba inayopendekezwa ni kuondelewa kwenye tunu za taifa mambo haya matatu Ibara ya 5: Uzalendo, uadilifu na uwajibikaji. Hoja ya msingi ikiwa kwamba kwa kipindi cha takribani miaka 10 tumepita katika misukosuko suko mingi ambayo inatokana na kukosekana utambuzi na ulinzi wa vipengele hivi vitatu.
Kumekosekana uzalendo kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali (hata raia) utendaji haujielekezi kwenye manufaa ya taifa na raia wake. Hii inaenda sambamba na kukosekana uadilifu katika matumizi ya ofisi na mamlaka waliopewa kama dhamana.
Na la tatu (uwajibikaji), watumishi wa wananchi wamesahau kuwatumikia wananchi na kutekeleza yaliyo ndani ya wajibu wao. Na iwapo wakithibitika kuwa wamekosea hakuna anayekubali kuachia nafasi, jambo ambalo linapoteza muda na raslimali.
Hivyo kukosekana na nguzo hizi tatu naliona ni pungufu kubwa sana ambalo kuzingatiwa kwake kungeifanya Tanzania ianze kurejesha heshima ya Tanzania kutokana na Viongozi na watumishi wa umma.

User avatar
Msechu
Posts: 36
Joined: Mar 11, 2015 16:03:14

Re: Ubora na Mapungufu ya Katiba Iliyopendekezwa

Apr 18, 2016 00:04:00

Naam Novat,

Pia kuondoa uwezo wa wananchi kuwawajibisha wabunge wao (Power of recall) kama ilivyokuwa kwenye Rasimu ni pungufu kubwa.

User avatar
idax
Posts: 2
Joined: Apr 15, 2016 23:04:15

Re: Ubora na Mapungufu ya Katiba Iliyopendekezwa

Apr 18, 2016 00:04:00

Novat wrote:

Hii ni hoja mujarabu, na inaakisi kipindi tulichomo sasa.
Maoni yangu ni kuwa katika utangulizi wa kuelimisha yaliyomo, inafaa kueleza japo kwa ufupi kuwa palikuwepo makosa ya kisheria katika hatua za Mchakato Katiba Mpya. Ibara ya 98 ilipaswa ifanyiwe kwanza merekebisho ili kutoa uhalali wa kuhuisha katiba.

Pungufu kubwa sana kwa Katiba inayopendekezwa ni kuondelewa kwenye tunu za taifa mambo haya matatu Ibara ya 5: Uzalendo, uadilifu na uwajibikaji. Hoja ya msingi ikiwa kwamba kwa kipindi cha takribani miaka 10 tumepita katika misukosuko suko mingi ambayo inatokana na kukosekana utambuzi na ulinzi wa vipengele hivi vitatu.
Kumekosekana uzalendo kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali (hata raia) utendaji haujielekezi kwenye manufaa ya taifa na raia wake. Hii inaenda sambamba na kukosekana uadilifu katika matumizi ya ofisi na mamlaka waliopewa kama dhamana.
Na la tatu (uwajibikaji), watumishi wa wananchi wamesahau kuwatumikia wananchi na kutekeleza yaliyo ndani ya wajibu wao. Na iwapo wakithibitika kuwa wamekosea hakuna anayekubali kuachia nafasi, jambo ambalo linapoteza muda na raslimali.
Hivyo kukosekana na nguzo hizi tatu naliona ni pungufu kubwa sana ambalo kuzingatiwa kwake kungeifanya Tanzania ianze kurejesha heshima ya Tanzania kutokana na Viongozi na watumishi wa umma.Hivi nyie wanasheria mnao uwezo/ruhusa ya kuwaelewesha wananchi kama katiba pendekezwa iko sawa na imezingatia maoni ya muhuimu yalio kuwepo kwenye rasimu ya Warioba? na kama ni ndio ifikapo kampeni mtafanya hivyo? na pia tuna tegemea maoni yenu kwa ujumla ya katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ambayo yataeleza kwa mchanganuo katiba pendekezwa imezingatia yale ya muhimu yaliokuwepo kwenye rasimu.

Tuna amini wanasheria kwa sasa mna mchango mkubwa saaana kwa taifa hili, Tuna hitaji kuona uwepo wenu zaidi.

User avatar
Msechu
Posts: 36
Joined: Mar 11, 2015 16:03:14

Re: Ubora na Mapungufu ya Katiba Iliyopendekezwa

Apr 18, 2016 00:04:00

idax wrote:

Hivi nyie wanasheria mnao uwezo/ruhusa ya kuwaelewesha wananchi kama katiba pendekezwa iko sawa na imezingatia maoni ya muhuimu yalio kuwepo kwenye rasimu ya Warioba? na kama ni ndio ifikapo kampeni mtafanya hivyo? na pia tuna tegemea maoni yenu kwa ujumla ya katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ambayo yataeleza kwa mchanganuo katiba pendekezwa imezingatia yale ya muhimu yaliokuwepo kwenye rasimu.

Tuna amini wanasheria kwa sasa mna mchango mkubwa saaana kwa taifa hili, Tuna hitaji kuona uwepo wenu zaidi.Mrina,

Ni kweli wanasheria wanapaswa kufanya zaidi katika mchakato wa Katiba. Chama kinajitahidi kwa rasilimali chache kilichonazo na kwa sasa upo uchambuzi wa katiba inayopendekezwa unaweza kuusoma na kushare na wengine

http://tls.or.tz/wp-content/uploads/2015/07/Ijue-Katiba-Inayopendekezwa-Booklet.pdf

User avatar
issakwisa6810
Posts: 1
Joined: Dec 7, 2016 17:12:03

Re: Ubora na Mapungufu ya Katiba Iliyopendekezwa

Dec 7, 2016 00:12:00

Mawakili wasomi,

Tukiwa manguli wa sheria hapa nchini, tunawajibu wa kutumia taaluma yetu kuwaelimisha wananchi na kushawishi maboresho (kama yapo) kwa katiba iliyopendekezwa kwa mustakabali wa taifa letu.

Tungependa kupata maoni yako binafsi kwa kuzingatia taaluma yako na bila kufungwa na itikadi za chama cha siasa au dini juu ya nini ubora na mapungufu ya katiba iliyopendekezwa.habari kaka mm ni mwanafunzi wa sheria tawi la udsm ukonga naomba msaada wako wa maelekezo unisaidie jinsi ya kujibu mitihani na mbinu mbalimbali pia kama itakupendeza unisaidie kwa baadhi ya mambo ya masomo,mm ndio niko ngazi ya cheti naomba msaada kwani naona giza